Wananchi katika kjiji cha Kisungamile kata ya matai wilayani Kalambo mkoani Rukwa wameiomba serikali kufanya marekebisho ya miundombinu ya maji ambayo imeharibiwa na mifugo na hivyo kupelekea kukosekana kwa huduma hiyo muhimu kwa zaidi ya mwezi mmoja na hivyo kulazimika kutumia maji ya visima ambayo ni hatari kwa afya zao.
Kijiji cha kisungamile kina zaidi ya wananchi elfumoja (1000) na kina patikana katika kata ya Matai , kijiji hiki kimekuwa kikikabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa huduma ya maji na huku wananchi wake wakilazimika kutumia maji ya mto Chimilango pamoja na maji ya visima ambayo si salama kwa afya zao na hivyo kulazimika kuitisha mkutano wa hadhara ili kujua hatima ya swala hilo.
Diwani wa kata hiyo Vitus Tenganamba amesema serikali inampango wa kuanzisha mradi mpya wa maji kwenye maeneo hayo na kuwataka wananchi kuendelea kuwa na subira wakati swala lao likiendelea kufanyiwa kazi. Mkuu wa wilaya hiyo Julieth Binyura amewataka wananchi kuacha kulima kwenye vyanzo vya maji kwa lengo la kuondokana na adha kuziba kwa mabomba hususani wakati wa masika. Inaelezwa kuwa chanzo cha kukatika kwa maji kila wakati kwenye maeneo hayo ni kutokana na wananchi kulima kwenye vyanzo vyamaji na huku maji yanayotoka yakiwa ni machafu muda wote.