Star Tv

Wizara ya afya nchini imeitaka halmashauri ya wilaya ya Rorya mkoani Mara kubomoa moja ya majengo mapya ya hospitali inayojengwa katika eneo hilo kutokana na kukosewa kwa ramani hatua inayoweza kusababisha hatari ya kuvujisha mionzi yenye athari kwa binaadam wakati wa utendaji kazi wake.

Hayo yametolewa katika taarifa kwa viongozi juu ya maendeleo ya mradi wa ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Rorya mkoani Mara mhandisi msimamizi wa majengo Joseph Aduol akisema kuwa jengo hilo lililokwisha jengwa itabidi kubomolewa ili kufuata ramani na matakwa ya kisheria ya majengo ya vyumba vya mionzi.  Amabapo Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Rorya Charles Chacha na mkuu wa wilaya hiyo Saimon Chacha nao pia wameonyesha jitihada walizozifanya katika kukabilina na tatizo hilo..

 

Baada ya kukagua na kujionea maendeleo ya ujenzi wa hospital ya wilaya hiyo mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Mara Samwel Kiboye anatoa Rai kwa watalaam katika wizara kutokuitia hasara serikali.

Hivi karibuni Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli alipokuwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Mara alitoa fedha kiasi cha shilling billion moja na million mia tano ili kuanza  ujenzi wa hospital ya wilaya ya Rorya.

 

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.