Gari Moshi ya mizigo iliyobeba shehena ya ngano iliyokuwa inatokea Dar es Salaam kuelekea mikoa ya kanda ya ziwa mpaka Kampala nchini Uganda imepata ajali usiku wa kuamkia Aprili kumi na tatu katika eneo la Kola Manispaa ya Morogoro na kusababisha adha kubwa kwa wasafiri wanaotumia njia hiyo kutokana na reli ya njia hiyo kung’oka kabisa.
Ajali hiyo inatajwa kutokea Majira ya saa mbili na robo Usiku na kusababisha njia hiyo ya reli kungoka na kusababisha treni nyingine kushindwa kupita katika eneo hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari mkuu wa kituo cha reli mkoa wa Morogoro Bwana Salvatory kimaro amesema gari moshi hiyo ilikuwa na injini namba C261 ilikuwa na behewa ishirini ambapo kati ya hazo mabehewa matano yaliancha njia na kuanguka ambapo amesema chanzo cha ajali hiyo hakijafahamika hata hivyo hakuna madhara yoyote yaliyotokea kwa binadamu amebainisha mkuu wa kituo.
Baadhi ya wakazi wa morogoro ambapo wameiomba serikali kuangalia kwa makini eneo kabla hayajatokea madhara kwa binadamu kwani limekuwa likisababisha ajali mara kwa mara jitihida za mafundi kurudisha tena njia hiyo ya treni ilikuwa ikiendelea .