Katika jitihada za kukabiliana na uvamizi wa tembo kwenye mashamba ya wananchi mkoani Rukwa, wakala wa hidfadhi za mistu wilayani kalambo wameanzisha mradi wa ufugaji nyuki ambao utasaidia wananchi kujikwamua na hali ya kiuchumi sambamba na kufukuza tembo kwenye mashamba yao.
Kumekwepo na malalamiko ya muda mrefu kutoka kwa wananchi wa kata za Kisumba na Pombwe wilayani Kalambo juu ya tembo kuvamia mashamba yao kisha kuharibu mazao na kupelekea serikali wilayani humo kupitia wakala wa hifadhi za misitu kubuni njia mpya ya kupambana na tembo hao kwa kuanzisha mradi wa ufugaji nyuki.
Hayo yameelezwa wakati akisoma akisoma risala fupi mbele ya kiongozi wa mbio za Mwenge Venansi Sinkala wakati wa uzinduzi wa mradi huyo unayo shirikisha vikundi vitano , amesema mizinga 100 yenye thamani ya shilingi million nane imekwisha kutundikwa tayari.
kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru, haji abdulla hamad amewashauri wananchi kuendelea kutumia mbinu mbadala za kutumia misitu kwa faida kama kufuga nyuki ili kutunza vyanzo vya maji ili kufikia malengo ya serikali ifikapo mwaka 2025.Awali akiupokea mwenge huo . mkuu wa wilaya ya Kalamnbo Julieth Binyura , amesema mwenge wa uhuru utazindua miradi 9 yenye thamani yua shilingi billion 1.2.