CHAMA cha kusafirisha viumbe pori hai nje ya nchi TWEA kimemuomba Rais Dkt; John Pombe Magufuli kuingilia kati sakata la kuzuiliwa kwa
biashara hiyo ili kuendelea na biashara baada ya kuzuiliwa na aliekuwa Waziri wa maliasili na utalii mwaka 2016 Prof Jumanne Maghembe.
Akiongea na wanahabari jijini Dar es salaam Katibu wa chama hicho ndugu Adam Waryoba amesema kuwa kitendo cha kuzuiliwa biashara hiyo
kimesababisha kukosa fedha za kigeni zikizokuwa zinapatikana kutokana na biashara hiyo. Aidha ameongeza kuwa viumbe wanavyovisafirisha nje ya nchi
havijazuiliwa kisheria. Baadhi ya watu wanaofanya biashara hiyo wakatumia fursa hiyo kueleza kilio chao kwa Rais Magufuli Miongoni mwa viumbe hao ni Jongoo, Vyura, Tumbili wasumbufu, Nyoka na wadudu ambao walikuwa wakipelekwa katika nchi zaidi ya 21 ulimwenguni ikiwemo Marekani, China na Uingereza.