Star Tv

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) leo tarehe 13 Machi 2019 amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa la nguvu za Atomiki Duniani (IAEA) Kanda ya Afrika Prof Shaukat Abdulrazak.

Katika Mkutano huo uliotuama kwa masaa kadhaa katika Ukumbi wa Wizara ya Kilimo Jijini Dodoma Waziri Hasunga amemueleza Prf Shaukat kuwa serikali ya Tanzania inaendelea na mchakato wa kubaini wafanyabiashara wanaouza mbegu feki kwa wakulima kwani wanasababisha hasara kwa wananchi na Taifa kwa ujumla wake.

Alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi Duniani ambazo wananchi wake wa wamekuwa wakiuziwa mbegu feki jambo ambalo serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt john Pombe Magufuli imetilia mkazo kadhia hiyo na watakaobainika watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Kadhalika, Waziri Hasunga alisema kuwa pamoja na Wizara ya Kilimo kuendelea na mchakato wa kuboresha kilimo kwa kutumia teknolojia mpya lakini bado inakabiliwa na uuzwaji wa viuatilifu feki jambo ambalo limefifihisha juhudi za wakulima kwa muda mrefu.

“Wananchi wetu wanajitahidi kulima kwa kiasi kikubwa lakini kumekuwepo na changamoto kubwa ya Viuatilifu na Mbegu feki jambo hili hatuwezi kuliacha kamwe hivyo hivi karibuni nimetangaza kiama na wafanyabiashara wanaosambaza tutakapowabaini tutawachukulia hatua kali sana” Alikaririwa Mhe Hasunga

Katika hatua nyingine alieleza kuwa wakulima wengi nchini wamekuwa wakitumia mazao yao kama mbegu badala ya kutumia mbegu mpya jambo hili linapunguza kwa kiasi kikubwa ufanisi katika uzalishaji wa mazao.

Akizungumza katika mkutano huo Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa la nguvu za Atomiki Duniani (IAEA) Kanda ya Afrika Prof Shaukat Abdulrazak alisema kuwa kukutana na waziri wa Kilimo nchini Tanzania kumeimarisha maradufu ushirikiano ambao umeanzishwa kwa muda mrefu na shirika hilo.

Alisema kuwa mradi wa nguvu za Atomiki Duniani katika Kanda ya Afrika unahusisha nchi 45 ambapo unajikita katika uhusiano wa ushirikiano katika mazao mbalimbali yanayozalishwa.

Alisema katika Visiwa vya Zanzibar Shirika hilo limesaidia kutatua changamoto kwa kuteketeza magonjwa yote yanayoambukizwa na Mbung’o.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.