Star Tv

Tanzania imetajwa na Benki ya Dunia kuwa miongoni mwa mataifa machache duniani ambayo yamefanikiwa pakubwa kupunguza pengo kati ya matajiri na maskini. Kwenye ripoti ya benki hiyo kuhusu usawa duniani, Tanzania imeorodheshwa pamoja na Cambodia na Brazil kama nchi tatu zilizopiga hatua sana.

Nchini Tanzania, ripoti hiyo inasema, ufanisi ulipatikana katika kipindi ambacho taifa hilo lilipata ukuaji thabiti wa uchumi wa kiwango cha wastani cha asilimia 6.5 kila mwaka kati ya 2004-2014. "Kiwango cha umaskini kitaifa kilishuka kutoka asilimia 34.4 mwaka 2007 hadi asilimia 28.2 mwaka 2012," ripoti ya benki hiyo inasema.

Kwenye kipimo cha pengo kati ya maskini na matajiri, Tanzania iliimarika kutoka alama 39 mwaka 2007 hadi chini ya alama 36 mwaka 2012. Kipimo cha wastani Afrika kusini mwa jangwa la Sahara mwaka 2015 kilikuwa alama 45.1.

"Hatua zilizopigwa na Tanzania katika kupunguza pengo kati ya maskini na matajiri kipindi hiki kifupi ni cha kutia moyo," Benki ya Dunia inasema. "Ushahidi unaonesha ufanisi huu ulitokana sana na ongezeko la matumizi miongoni mwa watu wa tabaka la chini."

Miongoni mwa asilimia 40 maskini, matumizi yaliongezeka kwa asilimia 3.4 ikilinganishwa na asilimia 60 wenye pesa ambao ongezeko lao la matumizi lilikuwa asilimia 1 pekee. "Ni wazi kwamba mambo yaliwaendea vyema zaidi watu maskini kuliko matajiri kipindi hiki," ripoti hiyo inasema.

Kuanzia mwaka 2007, kulikuwa na ongezeko katika biashara ya rejareja na viwanda, hasa vya vyakula, vinywaji na tumbao jambo ambalo benki hiyo inasema liliwezesha watu wasio na ujuzi sana kushiriki katika uchumi.

Kujitolea kwa serikali katika kuendeleza sera ambazo zinalenga kusawazisha mapato pia kumechangia Tanzania kupiga hatua, benki hiyo inasema. Moja ya sera hizi ni mkakati wa serikali wa kuimarisha kupatikana kwa huduma za msingi kama vile afya, elimu ya msingi, maji na usafi miongoni mwa watu maskini.

Pili ni Mfuko wa Maendeleo wa Tanzania ambao benki hiy inasema umesaidia jamii maskini kuweka akiba na kuwekeza hasa katika mifugo. Hata hivyo, benki hiyo imesema Tanzania inafaa kufanya juhudi zaidi kupunguza tofauti kati ya mikoa pamoja na kuimarisha upatikanaji wa huduma za kimsingi. Juhudi zaidi zinahitajika katika upatikanaji wa umeme na huduma za usafi.

Kwa hisani ya BBC

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.