Star Tv

Kampuni ya huduma za usafiri inayotumia programu tumishi Uber imetangaza mpango wa kuanzisha huduma za boti Tanzania. Kampuni hiyo kufikia sasa imekuwa ikitoa huduma za usafiri kupitia magari na bajaji. Huduma hiyo mpya itafahamika kama UberBoat. Meneja masoko wa Uber Kanda ya Afrika Mashariki, Elizaberth Njeri amenukuliwa na gazeti la Mwananchi akisema huduma zilizopo za Uber zimefanikiwa vyema na ndio maana wakaamua kuanzisha pia huduma ya boti.

Kadhalika, Dar es Salaam ni mji wa pwani pamoja na visiwa vya Zanzibar na hivyo usafiri wa boti utafaa sana. "Dar es Salaam imezungukwa na fukwe nzuri na visiwa vidogo vidogo lakini watu hawapati ladha halisi ya mandhari hayo kwa kuwa hawajui wanawezaje kufika huko. Huduma ya Uberboat ambayo inakaribia kuanza hivi karibuni itasaidia hilo," amesema Bi Njeri.

Hata hivyo, hakueleza ni lini huduma hiyo itaanza. "Siwezi kusema ni lini hasa, lakini ni 'very soon' (hivi karibuni) inaweza ikawa wiki mbili zijazo au mwezi mmoja lakini ndo hivi tumekwisha zindua. Hatutaishia Dar es Salaam na Zanzibar tu, tunatarajia kwenda na maeneo mengine kulingana na uhitaji wa soko."

Kampuni hiyo iliandaa tamasha kwa jina UberBOAT Party Jumamosi ambapo waliohudhuriwa walikuwa ni kwa mwaliko. Kwenye app ya kampuni hiyo, kulikuwa na bango la kiungo cha UberBoat ambapo waliotaka kuhudhuria tamasha hiyo walitakiwa kukitumia kujiandikisha.

Uber imekuwa ikiendesha biashara barani Afrika kwa takriban miaka mitano sasa. Kando na usafiri, kampuni hiyo imekuwa ikijihusisha katika biashara ya kusafirisha chakula kwa wakazi wa mijini ambapo wana huduma kama vile UberZenjiPizza ambayo ni huduma ya pizza ya Zanzibar na UberChoma ambayo ya nyama choma ikiwalenga wakazi wa Dar es Salaam.

Kampuni hiyo tayari ina huduma ya UberBoat katika maeneo mbalimbali duniani yakiwemo Croatia, Boston, Miami and Istanbul.

Kwa hisani ya BBC

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.