Star Tv

Marekani imejitoa katika baraza la haki za binaadamu la Umoja wa Mataifa na kulitaja kuwa na 'unafiki wa kisiasa na lenye upendeleo'.

"Taasisi hiyo ya "unafiki na upendeleo inakejeli haki za binaadamu", amesema mjumbe wa Marekani katika Umoja huo Nikki Haley.

Bi Haley mwaka jana alilishutumu baraza hilo kwa kuwa na "upendeleo mkali dhidi ya Israel" na kusema Marekani inatafakari uwanachama wake.

Baraza hilo lililoundwa mnamo 2006, lililo na makao yake Geneva limeshutumiwa kwa kuruhusu mataifa yenye rekodi yakutiliwa shaka ya haki za binaadamu kuwa wanachama.

Lakini wanaharakati wanasema hatua hiyo ya Marekani huenda ikaathiri jitihada za kuangalia na kushughulikia ukiukaji wa haki za binaadamu kote duniani.

Bi Haley alitangaza nia ya Marekani kujitoa katika baraza hilo katika mkutano wa pamoja wa waandishi habari kiwa na waziri wa mambo ya nje Mike Pompeo, aliyelitaja baraza hilo kuwa "mteteaji duni wa haki za binaadamu".

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa António Guterres, katika taarifa iliyotolewa kupitia msemaji wake, amejibu kwa kusema ange 'pendelea zaidi' kwa Marekani kusalia katika baraza hilo.

Kamishna wa haki za binaadamu katika Umoja wa mataifa Zeid Ra'ad Al Hussein, ameitaja hatua hiyo ya 'kusikitisha' na habari ya kushangaza mno".

Israel, kwa upande wake imepongeza hatua hiyo. Hatua hii ya sasa ya utawala wa Trump huenda ikawasumbua wale wanaoitazama Marekani kulinda na kushinikiza haki za binaadamu kote duniani.

Siku zote Marekani imekuwa na mzozano na baraza la haki za binaadamu la Umoja mataifa.

Utawala wa Bush uliamua kulisusia baraza hilo lililoundwa mnamo 2006 kwa sababu nyingi kama zinazotajwa na utawala wa Trump.

Balozi wa wakati huo wa Marekani katika Umoja wa mataifa alikuwa ni John Bolton - ambaye kwa sasa ni mshauri wa kitaifa wa masuala ya usalama wa rais Trump na mkosoaji mkali wa Umoja wa mataifa.

Ni mpaka miaka kadhaa baadaye, mnamo 2009, ndipo Marekani ilijiunga upya chini ya utawala wa rais Obama.

Washirika wengi wamejaribu kuishawishi Marekani isalie katika baraza hilo. hata wengi wanaokubaliana na shutuma za muda mrefu za Washington kuhusu taasisi hiyo na wanaamini kuwa Marekani inaweza kuwajibika kuigeuza kutoka ndani, badala ya kujitoa.

Umoja wa maatifa uliliunda baraza mnamo 2006 kuichukua nafasi ya kamisheni iliyokuwepo ya haki za binaadamu katika Umoja huo iliokabiliwa na shutuma kubwa kwa kuruhusu mataifa yenye rekodi duni ya haki za binaadamu kuwa wanachama. Kundi la mataifa 47 yaliochaguliwa kutoka maeneo tofuati duniani yanahudumu kwa muhula wa miaka mitatu katika baraza hilo.

UNHRC hukutana mara tatu kwa mwaka, na kukagua rekodi ya haki za binaadamu ya mataifa yote wanachama wa Umoja wa mataifa katika mpango maalum ambao baraza hilo husema hutoa nafasi kwa mataifa kusema walichokifanya kuimarisha haki za binaadamu.

Baraza hilo pia hutuma wataalamu wa kujitegemea na limeunda tume za uchunguzi kuripoti kuhusu ukioukaji wa haki za binaadmu katika nchi kama Syria, Korea kaskazini, Burundi, Myanmar and Sudan kusini.

Kwa hisani ya BBC.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.