Star Tv

Benki Kuu ya Tanzania(BoT) imezifutia leseni ya kufanya biashara benki tano na kuziweka chini ya ufilisi.

Taarifa iliyotolewa na BoT imezitaja benki hizo kuwa ni Covenant Bank For Women (Tanzania) Limited, Efatha Bank Limited, Njombe Community Bank Limited, Kagera Farmers' Cooperative Bank Limited, na Meru Community Bank Limited. BoT imeeleza kuwa imefanya hivyo kwa mamlaka iliyopewa chini ya kifungu cha 56(1)(g), 56(2) (a), (b) na (d), 58(2)(i), 11(3)(c) na (j), 61(1) na 41(a) cha Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006, Benki Kuu ya Tanzania imeamua kuzifunga; kusitisha shughuli zake zote za kibenki; kufuta leseni zake za biashara ya kibenki; na kuziweka chini ya ufilisi.

“Kwa mamlaka iliyopewa chini ya kifungu Na. 41(a) cha Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006; Benki Kuu ya Tanzania imeiteua Bodi ya Bima ya Amana (The DEPOSIT INSURANCE BOARD) kuwa mfiiisi kuanzia tarehe 04 Januari 2018,” imeeleza taarifa hiyo.” “Uamuzi huu umechukuliwa baada ya Benki Kuu ya Tanzania kujiridhisha kuwa benki hizi zina upungufu mkubwa wa mtaji kinyume na matakwa ya Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006 na kanuni zake. Upungufu huo wa mtaji unahatarisha usalama wa sekta ya fedha na kwamba kuendelea kutoa huduma za kibenki kwa benki hizo kunahatarisha usalama wa amana za wateja wake.”

Taarifa hiyo imeeleza kuwa BoT inapenda kuuhakikishia umma kuwa itaendelea kulinda maslahi ya wenye amana katika mabenki kwa lengo la kuleta uhimilivu katika sekta ya fedha.

Picha na mtandao.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.