Star Tv

Waziri mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa leo amewaongoza watanzania katika kutoa salamu za mwisho kwa watu 19, waliopoteza maisha kutokana na ajali iliyosababishwa na kudondoka kwa ndege katika mkoa wa Kagera wilayani Bukoba.

Salamu hizo za mwisho zimetolewa katika uwanja wa Kaitaba Wilayani Bukoba. Huku katika ajali hiyo watu 24 walinusurika na kuweza kuokolewa kutoka katika ndege hiyo ambayo ni mali ya kampuni ya usafirishaji ya Precision.Ndege hiyo iliyokuwa ikifanya safari zake kutokea Dar –es-salaam kuja Bukoba baada ya kuanguka ndani ya ziwa Viktoria kando na uwanja wa ndege wa Bukoba. Ajali hiyo ya ndege ilitokea majira ya saa mbili na nusu asubuhi tarehe 06/11, wakati ikitaka kutua katika uwanja wa ndege wa Bukoba. Huku serikali ikiahidi kugharamia mazishi ya waliopoteza maisha.

Latest News

Waziri Mkuu Akagua Visima Vya Dharura Dar Es Salaam
10 Nov 2022 13:31 - Kisali Shombe

 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua visima vya dharura vinavyosafishwa, kufufuliwa na kuunganishwa katika mfumo wa us [ ... ]

Waziri Wa Afya Aagiza Udhibiti Magonjwa Ya Mlipuko
09 Nov 2022 14:15 - Kisali Shombe

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ameagiza vituo vyote vya kutolea huduma za afya vya binafsi na serikali kuweka kituo maalum  [ ... ]

Vifo vitokanavyo na Utoaji wa Mimba usio salama, Kudhibitiwa
09 Nov 2022 13:21 - Kisali Shombe

Mpango wa idara ya afya wa kutoa elimu ya afya ya uzazi na matumizi ya uzazi wa mpango unatajwa kusaidia kupunguza mimba [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2023 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.