Star Tv

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala Bora na Serikali za mitaa (USEMI) ikiongozwa na Jaffari Chaurembo, Mbunge wa Jimbo la Mbagala haijaridhishwa na kasi ya Ujenzi wa Shule mpya maalum ya Sekondari ya Bweni na sayansi ya Wasichana katika Mkoa Kagera kupitia Mradi wa kuboresha Elimu ya Sekondari (SEQUIP).

Hayo yamebainishwa leo Oktoba 25, 2022 wakati Kamati hiyo ya USEMI ikipokea na kujadili taarifa kuhusu utekelezaji wa ujenzi wa shule mpya 10 za wasichana zinazojengwa katika mikoa 10 ya awali ambapo kila mkoa utajengewa shule moja.

“Leo tumepokea taarifa za ujenzi wa shule mpya katika mikoa 10, Wapo waliofikia asilimia 80 lakini Kamati imesikitishwa sana na Mkoa Kagera, ujenzi unaenda taratibu mno na bado wapo chini ya asilimia ambayo tuliitarajia”-Chaurembo.

Kwa Upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Angellah Kairuki amesema Serikali ilitoa Bilioni 3 kwa kila mkoa katika Mikoa 10 na ikaagiza kufikia tarehe 31 Disemba 2022 Ujenzi wa madarasa na miundombinu yote iwe imekamilika kwa viwango kulingana na miongozo iliyowekwa.

Latest News

Waziri Mkuu Akagua Visima Vya Dharura Dar Es Salaam
10 Nov 2022 13:31 - Kisali Shombe

 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua visima vya dharura vinavyosafishwa, kufufuliwa na kuunganishwa katika mfumo wa us [ ... ]

Waziri Wa Afya Aagiza Udhibiti Magonjwa Ya Mlipuko
09 Nov 2022 14:15 - Kisali Shombe

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ameagiza vituo vyote vya kutolea huduma za afya vya binafsi na serikali kuweka kituo maalum  [ ... ]

Vifo vitokanavyo na Utoaji wa Mimba usio salama, Kudhibitiwa
09 Nov 2022 13:21 - Kisali Shombe

Mpango wa idara ya afya wa kutoa elimu ya afya ya uzazi na matumizi ya uzazi wa mpango unatajwa kusaidia kupunguza mimba [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2023 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.