Star Tv

Watu wawili wamefariki Dunia na wengine ambao idadi kamili bado haijafahamika wamejeruhiwa baada ya kuibuka vurugu kati ya Askari Polisi na wakazi wa Kijiji cha Ikwambi kata ya Mofu wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro.

Kwa mujibu wa Mkuu wa mkoa wa Morogoro Fatma Mwasa amesema chanzo ni wakulima ambao ni wakazi wa kijiji hicho kuwafungia ndani ya ofisi ya Kijiji wenyeviti wa vitongoji, vijiji pamoja na Wafugaji kwa lengo la kutaka kuwachoma Moto wakiwatuhumu kushindwa kuwasaidia pindi wafugaji wanapoingiza mifugo katika mashamba yao.

Aidha watu wawili hao waliofariki ni Wakulima (mwanamke na mwanaume).

Miongoni mwa waliojeruhiwa ni Diwani wa kata hiyo Greyson Mgonela, ambaye baada ya kufanya mazungumzo naye kwa njia ya simu amesema wakati vurugu zinatokea wananchi walikuwa wakitumia silaha za jadi, Mawe, Mikuki na Marungu kuwapiga Askari, huku Askari nao wakitumia Mabomu ya Machozi na Kisha Risasi za Moto.

Latest News

Waziri Mkuu Akagua Visima Vya Dharura Dar Es Salaam
10 Nov 2022 13:31 - Kisali Shombe

¬†WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua visima vya dharura vinavyosafishwa, kufufuliwa na kuunganishwa katika mfumo wa us [ ... ]

Waziri Wa Afya Aagiza Udhibiti Magonjwa Ya Mlipuko
09 Nov 2022 14:15 - Kisali Shombe

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ameagiza vituo vyote vya kutolea huduma za afya vya binafsi na serikali kuweka kituo maalum  [ ... ]

Vifo vitokanavyo na Utoaji wa Mimba usio salama, Kudhibitiwa
09 Nov 2022 13:21 - Kisali Shombe

Mpango wa idara ya afya wa kutoa elimu ya afya ya uzazi na matumizi ya uzazi wa mpango unatajwa kusaidia kupunguza mimba [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2023 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.