Star Tv

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima, amewaomba wazee kubadilisha hadithi za kale walizo wasimulia wajukuu zao kuhusiana na Imani za kishirikina na badala yake wakawahadithie hadithi zitakazowajenga na kuwa raia wema kwa taifa.

Waziri Dkt. Gwajima ametoa kauli hiyo wakati wa Kongamano la Wazee kuelekea lililofanyika kwenye Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.

Dkt. Gwajima ameongeza kuwa, zipo baadhi ya Jamii, wakiona mzee macho yamekuwa mekundu na yanatoa Machozi na wengine wamezeeka na Migongo kupinda huibuka na dhana kuwa ni washirikina jambo ambalo sio la kweli.

"Wazee wangu niwaombe sana, kama kuna baadhi yenu waliwahi kuwahadithia wajukuu juu ya Habari za kishirikina huko nyuma na kuchochea Vitendo vya Ukatili basi ni wakati wa kuwabadili Fikra kwa kuwapa hadithi zitakazo wafanya kuwa Raia wema kwa Taifa lao"- Dkt. Gwajima.

Aidha Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Wazee Lameck Sengo ameiomba Serikali kuona suala la kuwashirikisha kwenye vyombo vya maamuzi linatekelezwa kwani kuwepo na uwakilishi katika vyombo hivyo husaidia wazee sauti yao kusikika.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.