Star Tv

Watu zaidi ya 236 wameugua Kipindupindu kwa kipindi cha zaidi ya Mwezi mmoja tangu Ugonjwa huo uingie katika Wilaya za Mbarali na Chunya Mkoani Mbeya na sasa umelipuka katika Wilaya ya Songwe na Momba mkoani humo.

Ugonjwa huo tayari umeenea katika baadhi ya Vijiji Wilayani Songwe Samweli Jeremia Opurukwa ni Mkuu wa Wilaya ya Songwe akizungumza na Wakuu wa idara na wanahabari pamoja na baadhi ya wananchi amesema tatizo hilo lipo hata hivyo hakuna vifo vilivyotokana na ugonjwa huo .

Pamoja na elimu kutolewa imeelezwa kuwa bado wananchi wanaonesha ukaidi katika kuzingatia ulaji wa vyakula serikali imeamua kuwachukulia hatua za kisheria, wale wote watakao pata ugonjwa huo pamoja na kuwekewa bendera nyekundu katika kaya itakayo kuwa na mtu anayeugua ugonjwa huo .

Mbali na serikali kuchukua hatua za kukabiliana na Ugonjwa huo pia wananchi wametakiwa kuchemsha maji ya kabla yakuyanywa pia wametakiwa kusitisha unywa ji pombe za kienyeji hata ammri ambayo utekelezaji wake ni mgumu wahusika wanatumia njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufunga mlango kwa kufuri kwa nje na ndani yake mambo ni kama kawaida.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.