Star Tv

Watu sita wamefariki dunia na wengine wanne wamejeruhiwa katika ajali iliyohusisha gari aina ya Toyota Noah iliyogongana na lori aina ya scania katika eneo la ALKATANI kata ya Sepeko tarafa ya Kisongo wilaya ya Monduli mkoa wa Arusha katika barabara ya Arusha Babati.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ACP. Justine Masejo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo amesema ajali hiyo imetokea jana Aprili 19, 2022 muda wa saa nne usiku na kuyataja magari hayo kuwa ni Toyota Noah yenye namba za usajili T.189 DFY iliyokuwa ikitokea Arusha mjini kwenda Karatu na lori lenye namba za usajili T.250 CAA ambapo lori hilo lilikuwa linatokea makuyuni kwenda Arusha mjini.

ACP. Masejo amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva ambapo alishindwa kulimudu gari hilo na kuhamia upande mwingine wa Barabara na kusabisha kugonga gari hilo aina ya toyota Noah. Kamanda Masejo amesema kuwa Jeshi hilo linamshikilia dereva wa roli aliyesababisha ajali hiyo.

Aidha amesema kuwa bado wanaendelea kufanya uchunguzi kufahamu majina halisi ya abiria waliofariki katika ajali hiyo na amewaomba wananchi kufika katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Arusha Mount Meru kutambua miili ya marehemu.

ACP. Masejo ametoa wito kwa watumiaji wa vyombo vya moto kuwa waangalifu wakati wamatumizi ya vyombo hivyo ili kupunguza ajali ambazo zinagharimu maisha ya watu.

Latest News

AMPELEKA MKWE MAHAKAMANI KWA KUMZUIA KUOLEWA.
17 May 2022 06:34 - Grace Melleor

Binti aliyefahamika kwa jila la Halima Yunusa Ibrahim amempeleka babamkwe wake latika Mahakama ya Kiislamu Islamic (Shar [ ... ]

WANAJESHI WA UKRAINE WALIOZINGIRWA WALIOKOLEWA.
17 May 2022 05:50 - Grace Melleor

Ukraine imethibitisha kwamba mamia ya wapiganaji wake waliokuwa wamekwama kwa zaidi ya miezi miwili katika mji wa Maurip [ ... ]

JESHI LA NATO KUANZA KUFANYA MAZOEZI KUKABILI VITA.
16 May 2022 09:23 - Grace Melleor

Mazoezi makubwa zaidi katika historia ya Baltics ya Muungano wa kijeshi wa NATO yanatarajiwa kuanza baadaye hii leo.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2022 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.