Abdurahman Kinana ataendelea kuwa katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania.
Bw Kinana amekuwa akishikilia wadhifa huko tangu serikali ya awamu ya nne, na wachambuzi wamekuwa wakimuona kama kiungo muhimu sana katika kuleta mabadiliko ndani ya Chama.
Uamuzi huo umetolewa na mwenyekiti wa chama hicho raisi John Magufuli na kutangazwa mbele ya wajumbe takribani 1,900 katika mkutano mkuu wa tisa wa chama hicho mjini Dodoma.
Uamuzi huo umepokelewa kwa furaha na wajumbe karibu wa chama hicho.
Picha na mtandao.