Star Tv

Miili ya waandishi wa habari watano pamoja na dereva wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza waliofariki katika ajali ya gari Januari 11 imeagwa leo Januri 12, 2022 katika uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.

Viongozi mbalimbali wa dini na serikali akiwemo Waziri wa Habari Nape Nnauye, Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi ni miongoni mwa wawalioshiriki katika zoezi hilo pamoja na wananchi.

Aidha kwa upande wake Wazir wa Habari Nape Nnauye ametoa siku saba kwa waajiri wanaodaiwa na waandishi wa habari waliofariki katika ajali ya gari wilayani Busega kuhakikisha wanalipa stahiki zao.

"Nimepewa salamu hapa kuwa miongoni mwa waliolala kwenye majeneza hapa mbele yangu kuna stahiki zao hawajalipwa, natoa siku saba kwa waajiri wote wanaodaiwa kulipa stahiki zote za marehemu na kutoa taarifa ofisi ya mkuu wa mkoa"- Alisema Waziri Nape

Nape amesema kuwa waajiri wanapaswa kukumbuka yeye ndiye mwenye leseni za vyombo vya habari hivyo wahakikishe wanakamilisha zoezi loa kulipa stahizi za wwanaodai.

"Yawezekana kuna hali ngumu ya kiuchumi, lakini nasema stahiki zote za marehemu hawa zilipwe ndani ya siku saba. Hayo ya hali ngumu tutayazungumza huko mbeleni kwa waandishi ambao wako hai ila kwa hawa marehemu lazima walipwe"-Aliagiza Waziri Nape

Idadi ya vifo vilivyotokana na ajali hiyo vimefikia 15 baada ya majeruhi mmoja aliyekuwa amelazwa katika hospitali ya rufaa ya Kanda ya Bugando kufariki dunia wakati akipatiwa matibabu.

Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando, Dkt. Fabian Massaga amesema hospitali hiyo ilipokea majeruhi sita wa ajali hiyo ambapo mmoja amefariki na wanne wanaendelea na matibabu huku mmoja akiwa ameruhusiwa kutoka hospitalini.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.