Siku moja baada ya aliyekuwa Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai kutangaza kujiuzulu, Bunge limetangaza kusitisha shughuli zake zote mpaka atakapopatikana spika mpya Februari mosi mwaka huu.
Katika taarifa iliyotolewa leo Ijumaa Januari 7, 2022 na Katibu wa bunge, Nenelwa Mwihambi imesema taratibu za uchaguzi wa kujaza nafasi ya Spika zinaendelea huku akitangaza kuahirishwa vikao vya Kamati za Bunge ambavyo vilipangwa kuanza wiki ijayo.
Kwa mujibu wa tangazo la katibu huyo wa Bunge kwa wabunge, amesema hakuna shughuli zitakazoendelea kwa kipindi ambacho nafasi ya Spika iko wazi hivyo amewaagiza wabunge wote kufika jijini Dodoma Januari 31, 2022 kwa ajili ya kuanza Mkutano we Sita wa Bunge utakaoanza Februari Mosi.