Star Tv

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Dorothy Gwajima ameanzisha utekelezaji wa mfumo wa kukusanya maoni toka kwa watendaji wa taasisi anazosimamia kuanzia makao makuu ya wizara idara zote mbili ya afya na maendeleo ya jamii.

Mfumo huu una lengo la kuwa na utaratibu wa ndani wa watendaji kutoa maoni dhidi ya mifumo ya uendeshaji wa taasisi zao ili kuboresha kwa uendelevu mpango mkakati wa kuimarisha mifumo ya uendeshaji wa Taasisi anazosimamia kwa ajili ya kuongeza ufanisi katika utendaji kazi wa watumishi wa sekta hiyo.

Amebainisha hayo leo Tarehe 14 Desemba 2021 Jijini Dodoma katika ofisi za Wizara ya Afya jengo la Bima ya Afya na baadaye Mji wa Serikali Mtumba wakati akiendesha zoezi hilo la kikao maalumu cha Mtumishi Sema na Waziri wa Afya kwa Maoni na Maboresho Mahala pa Kazi. Akirejea hotuba yake aliporiti kama Waziri kwenye sekta hiyo Disemba, 2020.

Dkt. Gwajima amesema kuwa zikiwa zimebaki siku chache kukamilisha mwaka 2021 ameona vema kufanya tathmini hii ili kujipanga vema zaidi kwa kutumia uzoefu wa mwaka mmoja wa utekelezaji kwa lengo la kwenda kasi zaidi na kufikia matarajio ya wananchi.

Amebainisha kuwa taasisi ya Afya zinatakiwa kuwa kimbilio kwa wananchi wanaofika kupata huduma kwa kufanya kazi kwa bidii kujituma na kujitolea ili kuepuka changamoto mbalimbali ambazo hutokea kwa kukosa mifumo imara ya uendeshaji.

“Ndugu watumishi hatua ya kwanza ya safari ya kwenda kwenye mfumo imara wa uwajibikaji wa pamoja inaanza na fikra ya pamoja kwamba ninalotamani mimi au sisi litokee liwe la wote. tusitake wateja tu ndiyo wafanye tathmini dhidi yetu bali hata sisi tufanyiane tathmini sisi kwa sisi kwa hoja na kwa nia njema ya kuboresha mifumo ya kiutendaji." Amesema Dkt Gwajima

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amemshukuru Waziri kwa utaratibu huo ambao amesema ni nadra katika taasisi kwa viongozi kupimana.

"Ni jambo la kihistoria kuwa na utaratibu huu kwani utasaidia kuwajenga watumishi wote kuwa na mtazamo mmoja kuanzia ngazi ya uongozi, mara nyingi viongozi huwa hawafahamu hali halisi ya changamoto za watumishi wa chini yao" amesema Dkt. Jingu.

Aidha kwa upande wake Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Sichalwe amemshukuru Waziri wa Afya Dkt. Gwajima kwa ubunifu aliouanzisha, huku akiwataka Watumishi waliojitokeza kuitumia fursa hiyo kama sehemu ya maboresho ili kuongeza ufanisi katika kuwahudumia wananchi.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.