Star Tv

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima ametatua kero sugu iliyodumu muda mrefu inayowahusu ndugu wanaouguza wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa Mkoa Amana Jijini Dar es Salaam.

Kero sugu imetolewa ufumbuzi mara baada ya watu waliokuwepo kulalamikia uamuzi wa uongozi kuruhusu ndugu mmoja tu kwa wagonjwa wote kuingia kumuona mgonjwa wao hata wenye uhitaji wa ndugu wawili kulingana na hali ya mgonjwa.

Dkt. Gwajima anetatua kero hiyo wakati akiwa katika mwendelezo wa ziara zake za kuhamasisha watumishi wa umma kuweka mikakati ya kuzungumza na wateja kila siku kwa lengo la kuboresha huduma kwa jamii kufuatia utekelezaji wa maelekezo yake kuwa kila kituo cha utoaji wa huduma za Afya hapa nchini kihakikishe kinaanzisha "saa ya kigoda cha sema na mteja boresha huduma".

Aidha Dkt.Gwajima amewataka watumishi wa umma kubadilisha mfumo wa utendaji kazi uwe wenye vishawishi kwa wateja ili wavutiwe kufuata huduma zinazotolewa kama sehemu ya kujiandaa na utekelezaji wa Bima ya Afya kwa wote

Kwa upande mwingine Dkt Gwajima ameelekeza kuwa, viongozi watoke maofisini wazungumze na wateja na wagonjwa ili wapate mitazamo yao kuhusu huduma kuwa wapi ziboreshwe.

Pia amewaasa kuepuka kukaa ofisini na kupanga mipango kwa kusubiri kuletewa taarifa mezani kwani mara nyingi hazina uhalisia hali inayosababisha kichelewesha huduma bora kwa jamii.

Mganga mkuu wa Hospital ya Rufaa Mkoa wa Amana Dkt. Bryson Kiwelu amesema hospitali ya amana imeanzisha mfumo wa ufuatiliaji wa huduma kwa wagonjwa hali iliyosaidia mapato kuongezeka kutoka wastani wa Shilingi Milioni 291 kwa mwezi hadi kufikia shilingi Milioni 383 kwa mwezi hali iliyosaidia upatikanaji wa Dawa kwa asilimia 97.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.