Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Novemba 29, 2021 ametembelea kiwanda cha kuchenjua madini cha ‘Giant Elution’ kilichopo Chunya Mkoani Mbeya.
Akizungumza baada ya kukagua uwekezaji katika kiwanda hicho ambacho kinamilikiwa na Mtanzania, Majaliwa ametoa wito kwa watanzania waendelee kuwekeza katika sekta ya madini.
Waziri Mkuu amesema kuwa sekta ya madini imeendelea kukua na kuiwezesha nchi kupata mapato.
Pia Majaliwa amewaagiza Maafisa madini wa mikoa wawatembelee wachimbaji wadogo ili kuwapa elimu ya namna bora ya uchimbaji pamoja na kuwatafutia fursa za mikopo ili waweze kukuza biashara zao.