Star Tv

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa amekutana na wachezaji pamoja na benchi la ufundi la timu ya taifa ya mpira wa miguu (Taifa Stars) na kuwaeleza kuwa Taifa linawaamini na bado wana nafasi kubwa ya kuitangaza Tanzania kimataifa kupitia vipaji vyao katika soka licha ya kupoteza mchezo dhidi ya timu ya taifa ya Congo.

Waziri Bashungwa ameyasema hayo leo Novemba 12, 2021, katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, alipokutana na ujumbe wa timu hiyo kabla ya kuanza safari kuelekea nchini Madagascar kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya timu ya taifa ya nchi hiyo, utakaochezwa siku ya jumapili Novemba 14, 2021.

Amesema licha ya kupoteza mchezo dhidi ya timu ya taifa ya Congo, lakini watanzania wanatamani kusikia timu yao ikifanya vizuri katika mchezo wao dhidi ya timu ya Madagascar.

“Ni kweli tumefungwa na Congo lakini Mchezo kati ya Taifa Stars na Madagascar ni wa muhimu sana kwetu kama taifa na kwa FIFA hasa katika kupanga madaraja ya timu zilizo bora duniani”- Alisema Waziri Bashungwa.

Kwa upande wake meneja wa timu ya Taifa Stars Nadir Canavaro amesema wana imani ya kufanya vizuri katika mchezo huo, akiomba Watanzania kuendelea kuwa na imani na timu yao na kuiombea ili ifanye vizuri katika mchezo huo.

Latest News

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Urusi Kuchagiza Maendeleo Afrika kupitia Nishati ya Nuklia na Madini ya Urani
12 Aug 2023 10:07 - Kisali Shombe

ROSATOM, taasisi ya nishati ya nyuklia ya serikali ya Urusi ambayo iliwaalika zaidi ya waandishi wa habari 15 kutoka nch [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.