Star Tv

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa amesema Serikali kupitia Wizara yake tayari imetangaza zabuni ya kimataifa, ya usanifu wa viwanja viwili vya kisasa mahususi kwa ajili ya michezo ya ndani (sports and arts arena), katika jiji la Dar es Salaam na Dodoma.

Waziri Bashungwa ametoa kauli hiyo wakati akizindua Ligi ya Taifa ya Mpira wa Kikapu iliyopewa jina la “CRDB BANK TAIFA CUP,” katika viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.

Amesema ili kuendelea kuimarisha michezo hususani michezo ya ndani (indoor games), Serikali inaendelea na mikakati ya kuhakikisha inajenga viwanja hivyo viwili kama sehemu ya uboreshaji wa miundo mbinu ya michezo hapa nchini.

Kwa Mujibu wa Waziri Bashungwa Mchezo wa kikapu ni moja kati ya michezo sita (6) iliyopewa kipaumbele na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa imani kuwa, ukifanyika uwekezaji wa kutosha mchezo huo unaweza kutoa fursa kwa vijana wengi wa kitanzania.

Awali akizungumza katika uzinduzi huo Rais wa Chama cha Mpira wa Kikapu Tanzania Phares Magesa amesema Chama hicho kinaendelea na jitihada mbalimbali katika kuhakikisha Mpira wa Kikapu unaendelea kukonga nyoyo za watazamaji.

Kwa upande wake afisa uendeshaji Mkuu wa Benki ya CRDB ambayo ni mdhamini mkuu wa ligi hiyo bwana Bruce Mwile, amepongeza hatua ya Serikali ya kukusanya asilimia tano kutoka kwenye michezo ya kubahatisha itakayopelekwa kwenye mfuko wa maendeleo ya michezo akisema kiasi hicho kinachokusanywa na serikali kwa ajili ya kutunisha mfuko huo kitasaidia kuinua michezo iliyopewa kisogo na watu wengi kwa sabau ya ukata kwenye michezo husika.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.