Star Tv

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa wito kwa Watanzania pamoja na wadau wa soka nchini kuungana kwa pamoja na kuhakikisha timu ya Taifa ya Tanzania ya mpira wa Miguu (Taifa Stars) inafanya vizuri kwenye michezo yote iliyobaki ili kufuzu kushiriki kombe la Dunia litakalofanyika nchini Qatar 2022.

Waziri mkuu Majaliwa ametoa wito huo leo Novemba 4, 2021 wakati akiongoza Kikao cha pamoja cha wadau wa soka Nchini katika ukumbi wa uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.

Kupitia kikao hicho Waziri Mkuu Majaliwa ameweka bayana namna ambavyo wadau wa Taifa Star wamechangia na kufikisha Shilingi Bilioni 1.6 ambazo zitatumika kuihudumia timu katika maandalizi ya mechi zilizobaki za kufuzu kombe la Dunia.

Akizungumza kwenye kikao hicho, Majaliwa amesema ni lengo la Rais Samia Suluhu Hassan kuhakikisha anakuza sekta ya michezo nchini na anataka kuona mafanikio katika timu za Taifa hivyo mikakati ya kuifanya timu ya Taifa ifanikiwe ni sehemu ya kutimiza malengo aliyoyaweka Rais.
 
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu ametoa wito kwa wamiliki wa viwanda, Taasisi za Umma na binafsi pamoja na wadau wengine kuendelea kujitokeza kuichangia timu ya Taifa ili iweze kuweka Historia ya kushiriki kombe la dunia kwa mara ya kwanza.
 
Baadhi ya wadau Walioshiriki katika kikao hicho ni pamoja na GSM, TAIFA GAS, AZAM, CRDB, NBC, LAKE OIL, STAR OIL, K4 SECURITY, KAMBIASO.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.