Star Tv

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa ameigiza Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) kuandaa mpango mkakati wa makusanyo ya mirabaha pamoja na takwimu za maeneo yanayotakiwa kulipa mirabaha na kuziwasilisha wizarani mwisho mwa mwezi Septemba.

Waziri Bashungwa ametoa agizo hilo leo Septemba 10, 2021 Jijini Dodoma katika kikao chake na Kikosi kazi cha kukusanya maoni ya wadau katika Kanuni ya Leseni na Maonesho kwa Umma ya 2021 kutoka COSOTA kikiwasilisha taarifa ya maoni ya wadau kwa kanuni hiyo.

"Katika kikao ambacho tutakutana baada ya wiki mbili hizi nje na mkakati huo lazima tujue tunakusanya kwa akina nani na wako wapi pamoja na idadi yao, pia ongezeni kasi ya ukusanyaji wa mirabaha Disemba tunatakiwa kutoa gawio kubwa,"-Alisema Bashungwa.

Amesisitiza kuwa anahitaji kupata makadirio ya makusanyo ya mirabaha hiyo kwa mwaka huu wa fedha na kuanzisha utaratibu ambao atakuwa akifuatilia hali ya makusanyo hayo kwa kila mwezi kwa kuhakikisha anapata taarifa.

Pamoja na hayo naye Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Pauline Gekul aliitaka COSOTA kuhakikisha inajipanga zaidi na kujenga utaratibu wa kushirikiana na mashirikisho na vyama vinavyosimamia maeneo ya kukusanya mirabaha ili kutengeneza mazingira rafiki ya zoezi hili la ukusanyaji.

Aidha, Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi alifafanua kuhusu suala la kukamilika kwa mfumo utaka kuwa ukihesabu na kutambua nyimbo zinazochezwa katika vituo vya Redio kuwa unatarajia kukamilika mwezi Oktoba na ndiyo utaanza kufanya kazi rasmi.

"COSOTA mna kazi kubwa ya kufanya na kuhakikisha mnakusanya fedha za kutosha ili gawio la mwezi Disemba liwe lenye hamasa kwa Wasanii wetu ni imani yangu kuwa kwa Kanuni hii mpya na viwango hivi mlivyopanga kuwa vinalipika kikubwa katika hili ni kuweka mifumo ya kiteknolojia ambayo itarahisisha makusanyo hayo,"- Alisema Dkt.Abbasi.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.