Star Tv

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba amewakaribisha Wawekezaji kutoka Jamhuri ya Kiarabu ya Misri kuwekeza na kufanya biashara na Tanzania kutokana na uwepo wa mazingira rafiki na fursa za uwekezaji.

Waziri nchemba ametoa rai hiyo mjini Cairo Misri, wakati wa Kongamano la Kimataifa la Ushirikiano la Misri (Egypt International Cooperation Forum) lililowakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo washirika wa maendeleo kutoka Benki ya Dunia, Benki ya Maendeleo ya Afrika, Benki ya Ulaya, Jumuiya ya Ushirikiano wa Uchumi na Maendeleo, Sekta Binafsi na Asasi za Kiraia.

Dkt. Mwigulu alisema kuwa kuna umuhimu wa kusisitiza kukuza mahusiano ya kimataifa hususan kwa nchi za kiafrika zinazoendelea na kuweka mikakati endelevu ya kupambana na athari za janga la UVIKO – 19, ili kukuza uchumi.

“Katika Kongamano hili tumejadilia namna bora ya kusaidiana katika mitaji hususani katika nchi zenye Taasisi za Kifedha zenye uwezo wakutoa fedha katika mazingira ya UVIKO-19 kutokana kuathiri shughuli nyingi za kiuchumi”, alieleza Dkt. Nchemba.

Aidha Dkt. Nchemba ameipongeza Wizara ya Ushirikiano ya Kimataifa ya Jamhuri ya Kiarabu ya Misri kwa kuandaa kongamano hilo kwa kuwa limeunganisha wadau kutoka sehemu mbalimbali duniani na kutoa fursa ya kuweza kujadiliana na kupeana uzoefu kwa lengo la kuleta maendeleo.

Kongamano la Kimataifa la Ushirikiano la Misri (Egypt International Cooperation Forum) linalofanyika kwa siku 2 limehudhuriwa na nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania, Malawi, Senegal, Kenya, Namibia na Zambia.

Latest News

UFARANSA YAZINDUA MAGARI YA UMEME HAPA NCHINI.
20 Oct 2021 15:31 - Grace Melleor

Waziri wa Biashara na uchumi nchini Ufaransa Franck Riester amezindua magari ya umeme yaliyoundwa na kampuni ya E-Motion [ ... ]

UHITAJI WA NYAMA WAONGEZEKA NCHINI.
20 Oct 2021 15:23 - Grace Melleor

Serikali imesema malalamiko yaliyojitokeza hivi karibuni ya kupanda kwa bei ya nyama nchini yanaashiria ukuaji wa sekta  [ ... ]

UGANDA YAZINDUA GARI LA KIVITA LILILOUNDWA NCHINI HUMO.
19 Oct 2021 18:03 - Grace Melleor

Jeshi la Uganda limezindua gari la kivita lililoundwa nchini humo.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.