Star Tv

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango hii leo Septemba 7, 2021 amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa wa kwanza wa Afrika na Umoja wa Nchi za “Carribbean” (Africa – CARRICOM Summit) uliofanyika kwa njia ya mtandao.

Akizungumza katika mkutano huo, Makamu wa Rais amesema nchi za afrika na za “Carribean” zinafanana katika masuala mbalimbali hasa katika nia ya kuhitaji maendeleo ya haraka hivyo kuwepo na ushirikiano baina nchi hizo kutaongeza kasi ya maendeleo pamoja na kuwa na sauti ya pamoja kwa manufaa ya mataifa yote ndani ya umoja huo.

Makamu wa Rais amesema Tanzania inaunga mkono mapendekezo ya kuwepo kwa siku maalum ya umoja huo pamoja kuziasa nchi washiriki wa mkutano huo kuendelea kutoa msukumo wa kupatikana kwa chanjo kusaidia mapambano dhidi ya ugonjwa wa corona katika nchi zinazoendelea zenye uhitaji mkubwa wa chanjo hiyo.

Mkutano huo umejadili ushirikiano katika maeneo mbalimbali ikiwemo Uchumi wa Bluu, Afya, Teknolojia Mabadiliko ya tabia ya nchi pamoja na kudhibiti ugojwa wa Corona.

Mkutano huo umehudhuriwa na wakuu wa nchi na serikali kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika na Carribean

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.