Star Tv

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima ameawata Maafisa Ustawi wa Jamii na Maafisa Maendeleo ya Jamii kote nchini kushirikiana kwa karibu na wadau kuibua changamoto za Jamii na kuzitafutia ufumbuzi.

Dkt. Gwajima amesema hayo mkoani Mwanza wakati alipomtembelea Mtoto Shamsa Ramadhan Yusuph ambaye alipatwa na changamoto ya kumuuguza Bibi yake Angelina Francis na kushindwa kwenda shule.

Waziri Dkt. Gwajima ampongeza Mmiliki wa Shule ya Awali na Msingi Eden, Charlote Mbabazi ambaye amejitolea kumsomesha na kumhudumia mtoto huyo shuleni hapo.

"Mimi nikushukuru sana umefanya suala la kizalendo sana kumsaidia mtoto huyu kwa kuhakikisha hakosi haki ya kupata elimu itakayomsaidia katika maisha yake"-Alisisitiza Waziri Dkt Gwajima.

Aidha Waziri Dkt Gwajima amefurahishwa na uwezo mkubwa alionao Mtoto Shamsa katika masomo yake ikwia ni muda mchache tangu apelekwe shuleni hivyo kuwataka waalimu waendelee kumsimamia na kumpa mafunzo yatayoendelea uwezo wake.

Wakati huo huo amelipongeza Shirika la Nitetee Foundation kwa kuibua suala la mtoto Shamsa kumuuguza Bibi yake na kutopelekwa Shule hivyo ameyataka Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kutimiza wajibu wao kwa kuwasaidia wenye shida mbalimbali na wanaohitaji msaada.

Pia Waziri Dkt. Gwajima ameyataka Mashirika yasiyo ya Kiserikali kutimiza matakwa ya usajili kama inavyoelekezwa katika miongozo ya uendeshaji wa kazi husika.

"Nawapa Siku 30 kwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na wale wanaotoa huduma katika Makao ya watoto kuhakikisha mnakamilisha taratibu za usajili" alisema Waziri Dkt Gwajima

Vilevile, amewataka wataalam katika ngazi zote kushirikiana na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kuhakikisha kwamba maisha ya watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi wanapata huduma stahiki.

Akiwa mkoani Mwanza Waziri Dkt. Gwajima ametembelea katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando alikolazwa Bibi wa Shamsa, Angelina Francis na kuwataka wahudumu wa Hospitali hiyo kuendelea kumwangalia na kuhakikisha anapata huduma zote zinazohitajika.

Bibi Angelina Francis akizungumza na Waziri Dkt. Gwajima ameshukuru kwa huduma anazozipata hospitalini hapo kwani zimemfanya apate nafuu na kupata matumaini ya kurejea katika afya njema.

Mtaalam wa magonjwa ya wanawake Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt. Fridolin Mujuni amesema mgonjwa anaendelea vizuri na wameshachukua vipimo vyote ili kuchunguza na kuona Bibi Angelina anasumbiliwa na nini na kuweza kumpatia matibabu yanayostahili.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.