Star Tv

Waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Dokta Doroth Gwajima ameviagiza vyombo vya Dola kumchukulia hatua askofu wa kanisa la ufufuo na uzima Josephat gwajima kumhoji kuhusu madai anayoyatoa dhidi ya chanjo ya uviko 19.

Waziri Dkt. Gwajima amemtaka Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima kuthibitisha tuhuma alizotoa dhidi yake kuhusu 'kupokea hongo' ili apokee chanjo ya COVID-19.

Dkt. Doroth amesema askofu Gwajima anapaswa kuthibitisha tuhuma hizo alizozitoa hivi karibuni na kuagiza kuviagiza vyombo vya dola kumchukulia hatua mara moja endapo atashindwa kuthibitisha tuhuma hizo.

"Ninaelekeza majeshi yote, ya polisi na TAKUKURU waende wakatumie sheria zao, wamuite awaeleze maana kwamba amesema pesa! pesa! mimi Mhe. Waziri wa afya na Rais wa Tanzania tumepigwa pesa pesa chanjo ziingie, sasa yeye si amajua alikuwa shahidi alikuwa anatuchungulia atutajie , atutajie na aliyetupa, na tulipokelea wapi na yeye alikuwa yuko wapi chini ya sheria ya TAKUKURU"-Dkt. Doroth Gwajima.

Waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Dokta Doroth Gwajima ameviagiza vyombo vya Dola kumchukulia hatua askofu wa kanisa la ufufuo na uzima Josephat gwajima kumhoji kuhusu madai anayoyatoa dhidi ya chanjo ya uviko 19.

Waziri Dkt. Gwajima amemtaka Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima kuthibitisha tuhuma alizotoa dhidi yake kuhusu 'kupokea hongo' ili apokee chanjo ya COVID-19.

Kwa mujibu wa ukurasa wa twitter wa wizara ya afya ya nchi hiyo, Askofu huyo anapaswa kuthibitisha tuhuma hizo alizozitoa hivi karibuni na kuagiza kuviagiza vyombo vya dola kumchukulia hatua mara moja endapo atashindwa kuthibitisha tuhuma hizo.

Waziri Gwajima ametoa agizo la kuhojiwa kwa Askofu Gwajima na vyombo vya dola leo Agosti 17, 2021 akiwa katika kijiji cha Kyatunge, Butiama, mkoani Mara, na kueleza kuwa Askofu Gwajima amekuwa akitoa taarifa za kupotosha kwa makusudi kuhusu chanjo ya corona.

Waziri Gwajima alisema Askofu Gwajima amekuwa akitoa kauli hizo zinazoivuruga serikali katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Covid 19.

Itakumbukwa kuwa Askofu Gwajima aliwaeleza waumini wake katika ibada ya Jumapili iliyorushwa kwenye mitandao ya kijamii kwamba daktari atakaye’shadadia’ suala la chanjo bila kufanya utafiti wa kina ikiwemo madhara yake ya muda mrefu na muda mfupi atakufa, nah ii ni mara baada ya zoezi la chanjo kuanza nchini.

Latest News

UFARANSA YAZINDUA MAGARI YA UMEME HAPA NCHINI.
20 Oct 2021 15:31 - Grace Melleor

Waziri wa Biashara na uchumi nchini Ufaransa Franck Riester amezindua magari ya umeme yaliyoundwa na kampuni ya E-Motion [ ... ]

UHITAJI WA NYAMA WAONGEZEKA NCHINI.
20 Oct 2021 15:23 - Grace Melleor

Serikali imesema malalamiko yaliyojitokeza hivi karibuni ya kupanda kwa bei ya nyama nchini yanaashiria ukuaji wa sekta  [ ... ]

UGANDA YAZINDUA GARI LA KIVITA LILILOUNDWA NCHINI HUMO.
19 Oct 2021 18:03 - Grace Melleor

Jeshi la Uganda limezindua gari la kivita lililoundwa nchini humo.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.