Star Tv

Pamoja na mikoa ya kanda ya Kaskazini kuwa na utajiri wa mifugo hususan Ng’ombe, inaelezwa kuwa kuna idadi ndogo ya wafugaji wanaotumia kinyesi cha mifugo hiyo kama nishati mbadala, yaani BIOGAS.

Kwa mujibu wa wataalamu wa masuala ya Nishati Mbadala, ng’ombe wawili tu wanatosha kumwezesha mfugaji kumiliki mtambo wa Biogas, na hivyo kuondokana na adha ya kupikia kuni na kuwasha vibatari kwa ajili ya mwanga; lakini takwimu za kitaifa zinaonesha kuwa, pamoja na utitiri wa mifugo iliyopo nchini, ni asilimia 0.3 tu ya kaya zenye ng’ombe zinazotumia nishati hiyo.

Ni kwa kuzingatia hali hiyo, taasisi inayojishughulisha na masuala ya maendeleo-TAHUDE, imeanzisha kampeni maalum ya kuhamaisha wananchi wa mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara kujenga mitambo ya Biogas, ambapo kwa kuanzia imepokea ruzuku ya fedha zaidi ya shilingi milioni 270, kutoka Taasisi ya serikali ya Marekani(USADF) inayosaidia maendeleo katika baadhi ya nchi za Afrika. Gilliard Nkini, ni Mratibu wa taasisi hiyo hapa nchini.

Utoaji wa elimu ya kutosha kuhusu manufaa ya matumizi ya Biogas, hususan kwa wale waishio vijijini, ni eneo litakalopewa kipaumbele wakati wote wa utekelezaji wa mradi huu utakaodumu kwa miaka mitatu.

Linda Lifiga kutoka Taasisi ya Diligent, ndiye mratibu wa miradi yote inayopata ruzuku ya USADF hapa nchini.

Dkt.Askwar Hilonga, mshindi wa Tuzo ya Kimataifa ya uvumbuzi wa chujio la maji la Nano Filter, ndiye muasisi wa mradi huo, unaolenga kubadili mtindo wa maisha ya wakulima na wafugaji.

Kwa mujibu wa masharti ya mradi huo, wanufaika watajengewa mtambo wa Biogas kwa mkopo ambao utalipwa katika kipindi cha uhai wa mradi huo.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.