Star Tv

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Robert Gabriel ameyataka mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo yanahusika na midahalo ya vijana kuhusu masuala ya amani nchini Tanzania na katika nchi za maziwa makuu kuzingatia sheria zinazoratibu usajili wa mashirika hayo.

Mkuu wa mkoa amebainisha hayo kupitia hotuba yake iliyowasilishwa na mstahiki Meya wa Mstahiki Meya Halmashauri ya Ilemela Renatus Mulungu kwa niaba yake katika ufunguzi wa mradi wa Mtandao wa vijana wa nchi za maziwa makuu kuhusu amani na usalama ambazo zinajumuisha nchi ya Tanzania, Rwanda, DR Congo na Uganda uliozinduliwa jijini Mwanza.

“Naona mradi huu unalenga kuchangia nguvu zake katika kutatua machafuko na kuleta amani na utulivu katika maziwa ambazo zimeharibika kutokana vita ya ndani, ghasia au machafuko….Dunia imeshuhudia machafuko, vita ghasia na migogoro katika maziwa makuu, hivyo ni wazi kuwa mradi huu utasaidia kuleta utatuzi na kuzifanya nchi hizo kupata maendeleo”- Amesema Mulunga.

Kwa upande wake mratibu wa Mratibu Mradi Mtandao wa Vijana nchi za Maziwa Makuu kuhusu amani na Utulivu nchini Tanzania Bwana Jimmy Luhende amesema mradi huo utawasaidia vijana kuwa mabalozi wa kuhamasisha amani na utulivu .

“Mradi huu umelenga nchi za maziwa makuu ambazo zimekuwa na machafuko kwa muda mrefu na sisi Tanzania, sisi ni mashahidi Tanzania tumepokea wakimbizi kutoka katika maeneo haya, kwahiyo mradi huu umelenga kuwaandaa vijana kuzungumza kuhusu mambo ya amani……”-Amesema Bwana Jimmy Luhende.

Aidha Meneja Mradi Mariam Aganze kutokea nchini DR Congo anasema kupitia mradi huu utasaidia vijana kuwa sauti ya upatikanaji wa amani na utulivu hususani katika nchi zenye machafuko.

Baadhi ya washiriki katika uzinduzi wa mradi huu wanaunga mkono wakiutazama katika mrengo chanya wenye kuleta amani na utulivu hususani kwa nchi zinazonufaika na mradi huu.

Ufunguzi huu wa Mradi huu umehudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo vijana 21 waliochaguliwa kutoka mikoa tofauti hapa nchini pamoja na maafisa maendeleo kutoka baadhi ya mikoa hapa nchini.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.