Star Tv

Rais Samia Suluhu Hassani amewataka wanawake nchini kujenga utamaduni wa kujiamini kwakuwa ukombozi wa mwanamke unaanza na mwanamke mwenyewe hasa katika kuchangamkia fursa mbalimbali za kiuchumi zilizopo katika jamii.

Rais Samia ametoa wito huo ikiwa ni mwendelezo wake wa kuzungumza na makundi mbalimbali tangu apate dhamana ya kuliongoza taifa ambapo safari hii amezungumza na wanawake wa mkoa wa Dodoma kwa niaba ya wanawake wote hapa nchini.

Samia amesema kutokana na utekelezwaji wa usawa wa kijinsia ambao unatekelezwa duniani kote ndio umesaidia wanawake kuonekana wanaweza katika nyadhifa za juu za maamuzi.

''Mafanikio makubwa yamepatikana katika eneo hili na mfano halisi ni mimi niliyesimama hapa, miaka 20,25,30 nyuma hatukuwa tukilitazamia hili, lakini leo imewezekana tuko hapa….idadi ya wanawake katika vyombo vya maamuzi imeongezeka''- Rais Samia.

Amesema serikali imeendelea kuongeza fursa za wanawake kupata ajira na amewataka wananchi hao kuhakikisha nawanatumia fursa hizo vema ili mwanamke awe amekombolewa katika Nyanja ya kiuchumi.

Kuhusu matukio ya ukatili wa kijinsia Rais Samia Suluhu Hasan ametumia jukwaa hilo kuwataka wanawake kutumia vizuri wingi wao ili kupambana na vitendo hivyo ambavyo bado vinaonekana kuwa tatizo kubwa linalochangiwa na visasi na mani potofu.

Aidha, Rais Samia amemuelekeza Waziri wa Afya, Dkt. Dorothy Gwajima kuweka mpango mzuri wa ndugu kulipa deni la hospitali ili ikitokea mgonjwa wao amefariki dunia wakati akitibiwa, maiti isizuiwe.

Amesema si sawa maiti kuzuiwa na kwamba ni muhimu ukawekwa utaratibu wa kulipa deni la matibabu wakati taratibu za msiba zikiendelea.

“Hili la Watu kudaiwa wakati mtu amefariki wekeni mpango vizuri, hata Kidini tunaambiwa mtu akidaiwa hazikwi mpaka deni lilipwe ila sio kwa deni la Serikali, haileti maana mtu amefiwa anawaza msiba, kusafirisha na kuzika halafu bado unazuia maiti, hili haliwezekani.Nakuelekeza Waziri hebu nendeni mkaweke mpango mzuri wa kulipa deni na sio kuzuia maiti.”-Samia

Aidha, kupitia kauli yake hiyo Rais Samia Amefafanua kuwa tamko lake la maiti kutozuiwa lisichukuliwe vibaya; “Wananchi muelewe sio kwamba deni lisilipwe bali uwekwe mpango mzuri na mmoja wapo ni kulipa wakati matibabu yakiendelea na muhimu zaidi ni kuwa na bima ya afya,”- Amesema Rais Samia.

Mkutano huo wa wanawake umeenda sambamba na kauli mbiu isemayo “Mwanamke ni nguzo ya maendeleo tujitambue, tujizatiti tutekeleze wajibu wetu”, ambao umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, wanawake kutoka Tanzania Bara na Visiwani.

Latest News

SHAMBULIO LA KUJITOA MHANGA LAUA WATU NANE SOMALIA.
25 Nov 2021 10:26 - Grace Melleor

Polisi nchini Somalia wamethibitisha vifo vya raia katika bomu lililotegwa ndani ya gari katika mji mkuu Mogadishu, tele [ ... ]

WAZIRI MKUU SWEDEN AJIUZULU SAA CHACHE BAADA YA KUTEULIWA.
25 Nov 2021 09:01 - Grace Melleor

Waziri Mkuu wa kwanza mwanamke kuwahi kushikilia wadhifa huo nchini Sweden amejiuzulu saa chache mara baada ya kuteuliwa [ ... ]

MTOTO WA GADDAFI AZUIWA KUGOMBEA URAIS LIBYA.
25 Nov 2021 07:13 - Grace Melleor

Mtoto wa aliyekuwa kiongozi wa Libya hayati Muammar Gaddafi ameenguliwa katika kinyang’anyiro cha kuwania uchaguzi wa  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.