Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewasili nchini Kenya kwa ziara rasmi ya kikazi ya siku mbili.
Ziara hii ya rais Samia ni muendelezo wa jitihada za Tanzania na Kenya kuboresha na kuendeleza uhusiano na ushirikiano baina ya nchi hizo mbili na ni ziara ya pili kwa rais Samia tangu alipochukua madaraka kutoka kwa hayati Dkt. John Magufuli.
Rais Samia anatarajia kufanya mazungumzo na mwenyeji wake, Rais Uhuru Kenyatta kisha atalihutubia Bunge la Kenya litakalojumuisha Wabunge wa Mabunge yote mawili.
Aidha, Rais Samia pia atahudhuria na kuhutubia mkutano wa jukwaa la wafanyabiashara wa Kenya na Tanzania utakaofanyika jijini Nairobi.