Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro mkoani Arusha imesema itachukua miaka mingi kwa mchanga unaohama katika eneo la Olduvai kutoka nje ya hifadhi licha ya kwamba umekuwa ukisogea kila wakati.
Hifadhi ya ngorongoro iliingia kwenye maajabu nane ya dunia katika mwaka jana na hii ni kutokana na kuwepo kwa vivutio vya kipekee licha ya wanyama wa aina mbalimbali wanaopatikana katika hifadhi hii kipo kivutio kingine cha kipekee cha mchanga unaohama kila wakati na hapa hofu inatolewa dhidi ya mchanga huo kutoweka.
Naibu Mhifadhi mkuu wa Ngorongoro ,Maurus Msuha amesema mamlaka hiyo ipo kwenye mchakato wa kuingia kwenye orodha ya maeneo yaliyohifadhiwa ambayo yatatambuliwa na UNESCO kujitangaza zaidi kimataifa.
Hifadhi ya Ngorongoro ni kati ya hifadhi zilizopo Afrika ambazo unaweza kuwaona Faru weusi na wenye umri mkubwa wa unaofikia hadi miaka 52.
Picha na mtandao.