Star Tv

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza siku 14 za maombolezo pamoja na bendera kupepea nusu mlingoti kufuatia kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya tano Dkt. John Pombe Maguful kilichotokea Machi 17,2021.

Makamu wa Rais ametangaza msiba huo kupitia Televisheni ya Taifa (TBC) ambapo amesema kuwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli amefariki Dunia kutokana na maradhi ya moyo.

"Rais alilazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Machi 06, akaruhusiwa Machi 07. Kabla ya kupelekwa Hospitali ya Mzena Machi 14,2021".-Alisema Makamu wa Rais.

Kufuatia msiba huu wa taifa, Makamu wa Rais ametangaza siku 14 za maombolezo ambapo pia amesema bendera zitapepea nusu mlingoti.

Marehemu Rais Magufuli alizaliwa Oktoba 29,1959,  Alichaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 2015 na amefarika Machi 17, 2021 katika hatamu ya awamu ya pili ya urais wake.
#RIPRaisJohnPombeMagufuli

Latest News

RAIS TSHISEKEDI ADHIBITI BARAZA LAKE JIPYA LA MAWAZIRI.
13 Apr 2021 18:22 - Grace Melleor

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jumatatu alitangaza baraza jipya la Mawaziri katika hatua ambayo inaimar [ ... ]

MALIPO YA NDEGE MPYA TATU YAKAMILIKA.
13 Apr 2021 18:04 - Grace Melleor


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema tayari serikali imekamilisha malipo ya ununuzi wa ndege mpya tatu.

WASAFIRI KUTOKA KENYA KUINGIA KARANTINI KWANZA IRELAND.
12 Apr 2021 13:43 - Grace Melleor

Wasafiri wanaoelekea Ireland kutoka Kenya watalazimika kujitenga kwa wiki mbili baada ya kuwasili katika nchi hiyo ya ba [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.