Star Tv

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imezipiga faini ya Shilingi Bilioni 38.1 kampuni sita za simu kwa kosa la kutofikia viwango vya ubora wa huduma kama ilivyoanishwa na kanuni za ubora wa huduma za mwaka 2018.

Mamlaka hiyo kupitia Mkurugenzi wa TCRA, James Kilaba amezielekeza kampuni hizo kutozipeleka fedha hizo TCRA badala yake wazitumie katika kuwekeza kuboresha ubora wa huduma ndani ya siku 90.

Kampuni hizo na faini zilizotozwa kwenye mabano ni Airtel (Sh. Bilioni 11.5), Tigo (Sh. Bilioni 13), Halotel (Sh. Bilioni 3.4), Vodacom (Sh. Bilioni 7.8), Zantel (Sh. Bilioni 1) na TTCL (Sh. Bilioni 1.3).

Mkurugenzi wa TCRA, James Kilaba amesema mamlaka hiyo ilipima ubora wa huduma za mawasiliano katika robo ya mwisho wa mwaka 2020 na kubaini watoa huduma hao hawakufikia baadhi ya vigezo vya viwango vya ubora.

Amesema kwa mujibu wa kanuni ya 20 ya kanuni za ubora wa huduma za mawasiliano, mtoa huduma anayeshindwa kufikia vigezo anatakiwa kulipa faini.

“TCRA imeazimia kwamba badala ya kulipwa fedha hizo, tuzielekeze kwa watoa huduma. Kila mtoa huduma atumie kiasi chake alichotakiwa kulipa, akiwekeze katika kuboresha huduma”-

Aidha, Kilaba amesema anatoa siku tisini kwa kampuni hizo kutimiza makubaliano ya faini hiyo kwani wamekubaliana kwa kusaini hati ya makubaliano maalum, na ikiwa kuna mtoa huduma atakayefanya kinyume, TCRA itachukua hatua zaidi za kiudhibiti na kisheria pasipo kutoa taarifa.

Latest News

RAIS MAGUFULI AWAONYA WAKANDARASI WANAOCHELEWESHA MIRADI.
24 Feb 2021 13:33 - Grace Melleor

Rais John Magufuli amezindua barabara ya juu eneo la Ubungo ambayo imepewa jina la Marehemu John Kijazi, ambaye alikuwa  [ ... ]

MWILI WA BALOZI WA ITALIA WASAFIRISHWA KWENDA ROMA.
24 Feb 2021 09:52 - Grace Melleor

Mwili wa balozi wa Italia aliyeuawa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika jaribio la utekaji nyara uliotibuka s [ ... ]

MWANASIASA WA UPINZANI WA RWANDA AUAWA.
22 Feb 2021 07:59 - Grace Melleor

Mwanasiasa wa upinzani na raia wa Rwanda anayeishi mafichoni nchini Afrika Kusini ameuawa kwa kupigwa risasi.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.