Star Tv

Vinyonga 74 wameokolewa na kupelekwa kwenye bustani ya wanyama ya nchini Austria baada ya kubainika wakiwa kwenye sanduku katika uwanja wa ndege wa Vienna.

Wanyama hao waligunduliwa na maafisa wa usalama baada ya picha ya ukaguzi ya X-Ray ya sanduku kutiliwa shaka, ndipo vinyonga 74 walikutwa wamefichwa kwenye soksi na mikebe.

Viumbe hao wangeuzwa kwa gharama ya dola za Marekani 44,970 kwenye soko haramu, maafisa wamesema. Mwanaume huyo mwenye miaka 56 aliyesafiri kutoka Tanzania alikamatwa baadaye.

Mtu huyo anaweza kutozwa faini ya mpaka kiasi cha Euro 6,000, Wizara ya Fedha imeeleza.

''Vinyonga wanaweza kujificha vizuri...lakini hawakufua dafu mbele ya picha za ukaguzi''-Wizara ilisema katika taarifa yake.

Wanyama baadaye walisafirishwa kwenda kwenye bustani ya wanyama ya Vienna, Schönbrunn, ambako walifanyiwa uchunguzi na wataalamu.

Vinyonga watatu hawakumudu safari, Taarifa ya Wizara hiyo imebainisha kuwa vinyonga hao wana umri wa kuanzia wiki moja na zaidi.

''Kwa mujibu wa wataalamu kwenye bustani hiyo, viumbe hao wanatoka kwenye milima ya Usambara, eneo la mazingira ya baridi"- Wizara ya fedha imeeleza.

Vinyonga walio hai wanatunzwa katika bustani ya Schönbrunn.

Naibu katibu mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii nchini Tanzania Allan Kijazi akizungumza na Gazeti la Mwananchi nchini Tanzania amesema wanazo taarifa kuhusu tukio hilo na kuwa wanafuatilia suala hilo.

Akinukuliwa na gazeti hilo Kijazi amesema ''mchezo mchafu umefanyika".

Amesema wanafuatilia kujua ni namna gani mtu huyo alipita katika viwanja vya ndege bila kukamatwa

''Tumewasiliana na wenzetu wa interpol ili wafuatilie, wahusika warudishwe nchini, wachukuliwe hatua na hao vinyonga warudishwe.'' Alilieleza Mwananchi.

Chanzo BBC Swahili.

Latest News

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Urusi Kuchagiza Maendeleo Afrika kupitia Nishati ya Nuklia na Madini ya Urani
12 Aug 2023 10:07 - Kisali Shombe

ROSATOM, taasisi ya nishati ya nyuklia ya serikali ya Urusi ambayo iliwaalika zaidi ya waandishi wa habari 15 kutoka nch [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.