Star Tv

Abiria wote kutoka Tanzania na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo hawataruhusiwa kuingia nchini Uingereza na katika mataifa ya Irish kuanzia saa kumi alfajiri," amesema Grant Shapps, Waziri wa Usafirishaji nchini Uingereza.

Kuanzia tarehe 22 Januari, saa kumi alfajiri wasafiri wote kutoka au wamepita nchini Tanzania ndani ya siku 10 hawataruhusiwi kuingia Uingereza na mataifa ya Irish, na wale ambao wana haki ya makazi nchini Uingereza na wanatoka Tanzania watahitaji kujitenga nyumbani kwao watakapowasili.

Katika masharti mapya nchini Uingereza dhidi ya Corona, lazima watu wabaki nyumbani au kutosafiri, pamoja na kutosafiri nje ya nchi labda tu ukiwa umeruhusiwa kwa kibali maalum kufanya hivyo.

Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo zimeongezwa kwenye orodha ya Uingereza ya nchi zilizopigiwa marufuku ya wasafiri wake kuingia nchini humo kama hatua ya kudhibiti maambukizo ya aina mpya ya virusi vya Corona vilivyogunduliwa nchini Afrika kusini.

Serikali ya uingereza imesema marufuku hiyo itaanza rasmi Jumamosi na itakuepo kwa muda wa wiki mbili.

Chanzo na BBC Swahili.

Latest News

RAIS MAGUFULI AWAONYA WAKANDARASI WANAOCHELEWESHA MIRADI.
24 Feb 2021 13:33 - Grace Melleor

Rais John Magufuli amezindua barabara ya juu eneo la Ubungo ambayo imepewa jina la Marehemu John Kijazi, ambaye alikuwa  [ ... ]

MWILI WA BALOZI WA ITALIA WASAFIRISHWA KWENDA ROMA.
24 Feb 2021 09:52 - Grace Melleor

Mwili wa balozi wa Italia aliyeuawa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika jaribio la utekaji nyara uliotibuka s [ ... ]

MWANASIASA WA UPINZANI WA RWANDA AUAWA.
22 Feb 2021 07:59 - Grace Melleor

Mwanasiasa wa upinzani na raia wa Rwanda anayeishi mafichoni nchini Afrika Kusini ameuawa kwa kupigwa risasi.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.