Viongozi wa bodi katika vituo vya afya wilayani Tarime mkoani Mara wameonywa kuacha tabia ya kununua dawa za binadamu katika maduka ya nchi jirani ya Kenya badala yake watumie ya hapa nchini yaliyoidhinishwa na serikali.
Ni katika kikao cha kuunda bodi ya afya katika Halmashauri ya wilaya ya Tarime mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Apoo Tindwa anakemea viongozi wa bodi watakao kiuka agizo la serikali katika manunuzi ya dawa.
Nae mganga mkuu wa Hosipitali ya Halmashauri ya wilaya ya Tarime Hamidu Adinani alieza kwamba lengo la uundwaji wa bodi hizi za afya ni kuboresha huduma za afya kwa jamii.
Katika kikao hiki viongozi wa bodi za afya wametakiwa kuwa mstari wa mbele kujiunga na kuhimiza wananchi kujiunga na mifuko ya bima za afya ili kupunguza tatizo la kukosa matibabu katika vituo vya afya.
Picha na mtandao.