Star Tv

Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe ametangaza kwamba amejiuzulu kutokana na sababu za kiafya.

Amesema kwamba hataki maradhi alionayo kuingilia kazi yake , na kuomba msamaha kwa raia wa Japan kwa kushindwa kukamilisha muda wake.

Ameugua kwa miaka mingi kutokana na ugonjwa wa vidonda vya tumbo lakini hali yake imekuwa mbaya zaidi katika siku za hivi karibuni.

Mwaka uliopita , alikuwa waziri mkuu wa Japan aliyehudumu kwa kipindi kirefu nchini Japan.

Mwaka 2007, alijiuzulu ghafla alipokuwa Waziri Mkuu kutokana na mapambano yake ya ugonjwa huo wa tumbo, ugonjwa hatari ambao ameishi nao tangu alipokuwa kijana.

Waziri Abe anatajwa kama Waziri wan chi hiyo aliyeimarisha sekta ya ulinzi nchini Japan na kuongeza matumizi ya kijeshi , lakini ameshindwa kubadilisha kifungu cha sheria kinachoruuhusu jeshi kulinda taifa hilo pekee.

Huku akiwa waziri mkuu aliyehudumu kwa kipindi kirefu zaidi, anawacha umaarufu wa kulifanya taifa la Japan kuwa thabiti na serikali yenye uwezo mkubwa ambayo iliruhusu sera ya kuimarisha uchumi.

Pia aliimarisha uhusiano na Marekani kwa kufanya urafiki na rais Trump mara kwa mara katika uwanja wa gofu, Ijapokuwa serikali ilikumbwa na kashfa, ikiwemo suala la upendeleo mbali na kuharibu makusudi rekodi za umma.

Wakati mlipuko wa corona ulipokumba taifa hilo , jibu lake alilaumiwa mara kwa mara kwa kuchelewa kuchukua hatua madhubuti na mtu ambaye hakuelewa kilichokuwa kikiendelea.

Bwana Abe alisema kwamba ataendelea kuhudumu hadi mrithi wake atakapopatikana, lakini kufuatia tangazo lake la kujiuzulu litasababisha kupigwa kwa kura ndani ya chama cha LDP ili kutafuta mrithi wake.

Chama chake kitaamua Jumanne ijayo jinsi ya kufanya uchaguzi , kulingana na ripoti za chombo cha habari cha Kyodo.

 

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.