Star Tv

Mitandao ya kijamii Facebook na Twitter imemuadhibu Rais Donald Trump na kampeni yake kwa kutuma ujumbe ambapo rais huyo alidai watoto ''wanakaribia kuwa na kinga kamili'' ya virusi vya corona.

Facebook ilifuta ujumbe huo wa sauti kutoka kwenye mahojiano aliyoyafanya na kituo cha habari cha Fox News - ikisema kuwa ujumbe huo una "ujumbe wenye madhara wa taarifa za kupotosha kuhusu Covid- 19 ".

Huku Twitter ilifuatia ikisema kuwa imefunga akaunti ya kampeni ya Trump hadi ujumbe wake wa sauti sawa na huo ulipoondolewa.

Msemaji wa Facebook Jumatano jioni alisema;"Video hii ina madai ya uongo kwamba watoto wana kinga ya COVID-19 jambo ambalo ni ukiukaji wa sera zetu juu ya taarifa potofu zenye madhara kuhusu COVID."

Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa kampuni hiyo kubwa ya mtandao wa kijamii kuchukua hatua ya kuondoa ujumbe uliotumwa na rais kwa misingi ya sera yake juu ya taarifa potofu kuhusu virusi vya corona, lakini si mara ya kwanza kumuadhibu Bwana Trump kutokana na ujumbe aliotuma kwenye ukurasa wake.

Baadaye Jumatano, Twitter ilisema iliisitisha akaunti ya Trump @TeamTrump -kwasababu ilituma sehemu hiyo hiyo ya mahojiano, ambayo ukurasa wa Trump ulishirikisha Umma.

Msemaji wa Twitter alisema kuwa tweet ya @TeamTrump " inakiuka sheria za Twitter kuhusu taarifa za kupotosha kuhusu COVID-19 ".

Mwezi uliopita Twitter ilizuia kwa muda akaunti ya mtoto wa Trump , Donald Jr, kwa kushirikisha Umma taarifa ambayo ilisema kuwa ilichochea ''taarifa potofu'' kuhusu virusi vya corona na dawa ya hydroxychloroquine.

Lakini mwaka huu mwezi Machi, Twitter ilisema kuwa ujumbe wa tweeter uliotumwa na mjasiliamali Elon Musk ukidai watoto "wana kinga " kwa virusi vya corona haukuvunja sheria.

Akizungumza kwa njia ya simu na kipindi cha asubuhi cha Fox na marafiki Jumatano, Bwana Trump alidai kuwa ulikuwa muda wa kufungua shule zote nchini humo.

Rais Trump alisema: ''Ukiwatazama watoto na ninaweza kusema kabisa kwamba -wana kinga dhidi ya ugonjwa wa Covid-19, Ni wachache sana, wana kinga imara, ni vigumu kuamini, sijui jinsi unavyohisi kuhusu hili, lakini wana mfumo wa kinga imara sana kuliko sisi kwa ugonjwa huu.''

Bwana Trump, ambaye anagombea urais tena mwezi Novema, pia alisema kuhusu virusi vya corona bado ni janga ambalo limekosa ufumbuzi wa haraka.

Latest News

MIILI YA WATOTO 10 WALIOFARIKI KWA AJALI YA MOTO KYERWA YAAGWA LEO.
18 Sep 2020 10:38 - Grace Melleor

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Dkt.Bashiru Ally ameongoza mamia ya waombolezaji kuaga miili 10 ya wanafunzi waliofar [ ... ]

“MSAIDIZI WA BENARD MEMBE HAJATEKWA, ANASHIKILIWA NA POLISI” –-KAMAMDA MAMBOSASA...
17 Sep 2020 12:58 - Grace Melleor

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es salaam, SACP Lazaro Mambosasa amesema Jerome Luanda ambaye ni msaidizi wa Bernard  [ ... ]

WAZIRI MKUU WA LIBYA KUACHIA NGAZI MWISHONI MWA OKTOBA MWAKA HUU.
17 Sep 2020 12:30 - Grace Melleor

Waziri Mkuu wa Libya Fayez el-Sarraj ametangaza kuachia wadhfa wake wa uwaziri mkuu mwishoni mwa mwezi Oktoba 2020.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.