Star Tv

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson anatarajiwa kurejea ofisini kesho Jumatatu baada ya kupona maambukizi ya virusi vya corona.

Taarifa ya kiongozi huyu kurejea ofisini imethibitishwa na msemaji wa serikali ya Uingereza kupitia shirika la habari la DPA.

Johnson alikuwa katika makazi yake yaliyoko nje ya London baada ya kuruhusiwa kutoka hospitali ya Mtakatifu Thomas Aprili 12 alikolazwa kwa wiki nzima akitibiwa COVID-19.

Kulingana na shirika la habari la Uingereza la Press Association, siku ya Ijumaa Johnson alikutana na mawaziri waandamizi wa baraza lake kwa masaa matatu ikiwa ni pamoja na Waziri wa mambo ya Kigeni Dominic Raab aliyekaimu nafasi yake wakati akiwa mgonjwa.

Hata hivyo Johsnon anarejea katika wakati ambapo taarifa nyingi zikiripoti juu ya shinikizo linaongezeka dhidi ya serikali la miito ya kulegezwa vizuizi vya mapambano dhidi ya janga la corona.

 

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.