Star Tv

Waziri wa Ulinzi wa Sudan, Luteni Jenerali Jamaleldin Omar, amefariki  kufuatia mshtuko wa moyo akiwa Sudan Kusini wakati akishiriki katika mazungumzo ya amani baina ya serikali na waasi mjini Juba.

Katika taarifa siku ya Jumatano, Jeshi la Sudan limesema, Omar alikuwa mwanachama wa baraza la kijeshi lilolochukua madaraka baada ya kupinduliwa Omar al Bashir mwaka uliopita.

Imedokezwa kuwa, Omar alishiriki katika mazungumzo yaliyoendelea hadi Jumanne usiku na aliaga dunia usiku wa kuamkia leo, bado hakuna taarifa zaidi zilizotolewa kuhusu kifo cha Waziri hiyo.

Mazungumzo ya wawakilishi wa serikali ya Sudan na viongozi wa makundi ya waasi yalianza upya katika mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba Oktoba mwaka jana.

Mazungumzo hayo ya amani yalianza kufuatia mwito wa nchi za eneo kwa pande hizo kuonyesha nia ya kisiasa ya kutatua mgogoro ambao umekuwa ukitokota nchini humo kwa muda mrefu.

Wakati huo, serikali ya Sudan ilijipa miezi sita kufikia mkataba kamili wa amani, Kwa upande wake Waziri Mkuu wa serikali ya mpito ya Sudan Abdallah Hamdok alisema nchi yake inahitaji kupata amani ya kudumu ni kipaumbele cha serikali anayoiongoza.

                  Mwisho.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.