Rais wa Marekani Donald Trump pamoja na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu wamefunguliwa mashtaka ya kuhusika na jinai dhidi ya binadamu.
Raia kadhaa wa Marekani na Palestina wamefungua mashtaka dhidi ya viongozi wa Marekani na Israel ya 'kuunga mkono na kuhamasisha utendaji jinai za kivita na jinai dhidi ya binadamu' katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.
Kundi moja la raia wa Marekani na Palestina limewasilisha mashtaka hayo katika mahakama ya shirikisho ya Marekani dhidi ya Rais Donald Trump wa Marekani, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu pamoja na mkwe wa Trump Jared Kushner,.
Mashtaka hayo waliyofunguliwa ni kutokana na kile kinachojulikana kama viongozi hao wanaunga mkono na kuhamasisha utendaji wa makossa ya jinai za kivita na jinai dhidi ya binadamu katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina.
Raia hao wa Marekani na Palestina wamefungua mashtaka hayo katika kitengo cha mahakama ya shirikisho ya Marekani cha mji wa Columbia katika jimbo la Carolina ya Kusini.
Itakumbukwa kuwa tarehe 28 ya mwezi uliopita wa Januari Rais Donald Trump wa Marekani na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu walizindua mpango walioupendekeza wao wenyewe kuhusu Palestina walioupa jina la 'Muamala wa Karne'.
Mpango huo ujulikanao kama wa 'Muamala wa Karne' vilevile unasemekana kuwa umeupuuza mpango wa mapatano wa Waarabu unaojulikana kama mpango wa Mfalme Abdullah pamoja na mapatano ya Oslo yaliyofikiwa kati ya Harakati ya Ukombozi wa Palestina na utawala wa Israel.
Mwisho.