Star Tv

Baada ya uchaguzi wa hapo jana, majimbo ya Brandeburg na Saxony mashariki mwa Ujerumani yanaelekea kuunda serikali za vyama vitatu.

Katika jimbo la Brandenburg, waziri mkuu Dietmer Woidke anatazamiwa kuipanua serikali ya chama chake cha SPD pamoja na kile cha mrengo wa shoto kwa kukijumlisha chama cha Kijani. Na katika jimbo la Saxony ambako chama cha CDU chini ya waziri mkuu Michael Kretschmar kimeongoza na SPD, vyama hivyo vinatazamiwa kuungana na chama cha Kijani. Mfungamano na chama cha kijani katika serikali za majimbo hayo sasa ni wa lazima ili kuzuia ushiriki wa chama cha mrengo mkali wa kulia cha AfD katika serikali. Katika uchaguzi wa jana chama hicho cha mrengo mkali wa kulia kilishika nafasi ya pili katika majimbo yote mawili. Hata hivyo chama cha CDU kilishika nafasi ya kwanza katika jimbo la Saxony na chama cha Social Demokratik kiliongoza katika jimbo la Brandenburg.

CHANZO: Idhaa ya Kiswahili DW

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.