Kiongozi wa chama cha UKIP Henry Bolton anasema kuwa amesitisha uhusiano na mpenzi wake baada ya yeye kuripotiwa kutoa maoni ya ubaguzi wa rangi kumhusu Meghan Markle.
Alisema kuwa mapenzi yao hayataendelea akiwa na wajibu kama kiongozi wa chama lakini hana nia ya kujiuzulu.
Jo Marney alikuwa ametuma ujumbe wa simu kuwa watu weusi wana sura mbaya na mpenzi wake Prince Harry ataichafua familia ya kifalme.Bw Bolton alisema kuwa ilikuwa kinyume na katiba ya chama cha UKIP kuonyesha fikra zozote za ubaguzi wa rangi.