Star Tv

Ubalozi wa Uingereza na Taasisi ya Mercy Corps pamoja na Chuo kikuu cha Dar es salaam kimetoa mafunzo ya namna gani ya kukabiliana na majanga mbalimbali yanayotokea katika jamii na namna ya kukabilina nayo ikiwa ni pamoja na mawasiliano pale dharura inapotokea.

Mratibu wa shirika la Mercy Corps Nchini Anthony Sarota wakati akitoa maelezo juu ya namna ya kukabiliana na majanga hayo amesema wameamua kutoa mafunzo hayo kwa Jeshi la Polisi ili kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia hasa kwa upande wa mawasiliano pale majanga yanapotokea.

Aidha kwa upande wake Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP. Thabitha Makaranga ambaye pia ni mratibu wa mafunzo hayo kwa upande wa Jeshi la Polisi, amesema Jeshi hilo linashukuru wawezeshaji wa mafunzo hayo kwani yataleta tija na ufanisi wa kukabiliana na majanga ya dharura pindi yanapo tokea.

Kamishina wa Kamisheni ya Uchunguzi wa Kisayansi katika Jeshi la Polisi CP. Shaban Hiki akiongea katika hafla ya kufunga mafunzo hayo leo ambayo yamefanyika jijini Dar es salaam kuanzia Oktoba 10 hadi leo Oktoba 14, 2022 chini ya ufadhili wa ubalozi wa uingereza, taasisi ya mercy corps pamoja na wawezeshaji kutoka chuo kikuu dar es salaam amesema mafunzo hayo yatasaidia kuwajenga askari kiutendaji.

Latest News

Waziri Mkuu Akagua Visima Vya Dharura Dar Es Salaam
10 Nov 2022 13:31 - Kisali Shombe

¬†WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua visima vya dharura vinavyosafishwa, kufufuliwa na kuunganishwa katika mfumo wa us [ ... ]

Waziri Wa Afya Aagiza Udhibiti Magonjwa Ya Mlipuko
09 Nov 2022 14:15 - Kisali Shombe

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ameagiza vituo vyote vya kutolea huduma za afya vya binafsi na serikali kuweka kituo maalum  [ ... ]

Vifo vitokanavyo na Utoaji wa Mimba usio salama, Kudhibitiwa
09 Nov 2022 13:21 - Kisali Shombe

Mpango wa idara ya afya wa kutoa elimu ya afya ya uzazi na matumizi ya uzazi wa mpango unatajwa kusaidia kupunguza mimba [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2023 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.