Mazishi ya Malkia Elizabeth II aliyekuwa kiongozi mkuu wa taifa la Uingereza ambaye alifariki Septemba 08, 2022 yatafanyika leo Septemba 19, 2022 jijini London nchini humo.
Mwili wake utasafirishwa kwanza hadi Westminster Abbey kwa ibada ya kidini mbele ya maelfu ya watu, na kisha kuelekea kasri la Windsor kwa ibada ya kifamilia na watu wa karibu zaidi, hatimaye, maziko ya kibinafsi.
Wakuu wa nchi kutoka sehemu mbalimbali ulimwenguni wamekuwa wakiwasili kuungana na washiriki wa familia ya Kifalme kukumbuka maisha na huduma ya Malkia.
Wanachama wa familia za kifalme kutoka kote Ulaya, ambao wengi wao walikuwa ndugu wa damu wa Malkia wanatarajiwa kushiriki katika mazishi hayo akiwemo Mfalme Philippe wa Ubelgiji na Malkia Mathilde, Mfalme Felipe wa Uhispania na Malkia Letizia.
Aidha pia viongozi mbalimbali kutoka Afrika tayari wamewasili akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.