Star Tv

Mfalme Charles wa III wa Uingereza anakwenda Scotland leo kuungana na ndugu, jamaa na waombolezaji wengine ili kuhudhuria ibada ya kumwombea mama yake, Malkia Elizabeth wa II aliyeaga dunia wiki iliyopita.

Hii leo jeneza lenye mwili wa Malkia Elizabeth litapelekwa kwenye kanisa kuu la mtakatifu Giles mjini Edinburgh ambako kutakuwa na ibaada maalum na tukio la kuwasha mishumaa litakalohudhuriwa na familia ya kifalme wakiongozwa na Mfalme Charles. Mwili wa Malkia Elizabeth utalala ndani ya kanisa hilo kabla ya kusafirishwa kwenda mjini London hapo kesho kwa maandalizi ya kuugwa rasmi na kisha mazishi yake kufanyika mnamo Septemba 19. Hapo jana mamia kwa maelfu ya watu walijipanga barabarani kutoa heshima kwa mwili wa Malkia Elizabeth wakati msafara ulioubeba jeneza lake ulipokuwa njiani kutoka kasri la Balmoral kuelekea mji mkuu wa Scotland, Edinburgh.

 

CHANZO; DW SWAHILI

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.